+255 757 999 908
info@tawoma.or.tz
Follow Us:

MADINI YACHAGIZA MAENDELEO SEKTA YA AFYA

MADINI YACHAGIZA MAENDELEO SEKTA YA AFYA

Dkt. Biteko akabidhi Zahanati, Jengo la Mganga Mkuu na Gari la kubebea wagonjwa
 

Katika kuifungamanisha Sekta ya Madini na sekta nyingine, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amekabidhi kwa Serikali Zahanati, Nyumba ya Mganga Mkuu na Gari la kubebea wagonjwa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 312.5.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Kijiji cha Nyamishiga kilichopo Kata ya Lunguya katika Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga baada ya Kikundi cha Mshikamano kilicho chini ya Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake @_tawoma  kutoa mchango huo kwa Serikali kama mchango wake kwa jamii katika maeneo yanayokuzunguka mgodi.

Aidha, Dkt. Biteko ameipongeza TAWOMA kwa kuchangia maendeleo katika Sekta ya Afya na kuwataka waendelee kutoa mchango zaidi katika huduma mbalimbali za kijamii na kutoa wito kwa wamiliki wengine wa leseni kuchangia maendeleo katika jamii zinazowazunguka shughuli za madini.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini kuungana, kupendana na kushirikiana ili kufanya shughuli zao kwa amani na upendo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amekishukuru Chama cha Wachimbaji Wadogo Wanawake kwa kuona umuhimu wa kuchangia maendeleo ya jamii katika eneo wanalofanyia shughuli zao za uchimbaji madini.

Mndeme amewataka Wanawake kuendelea kuchapa kazi kwa lengo la kujiletea maendeleo na ametoa wito kwa wanawake wote nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini ili kuongeza kipato na kuepuka kuwa tegemezi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWOMA Semeni Malale amesema Kikundi cha Mshikamano TAWOMA kimechangia zaidi ya Shilingi milioni 289 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Zahanati, jengo la nyumba ya Mganga Mkuu na Ununuzi wa gari la kubebea wagonjwa wa dharura katika kijiji cha Nyamishiga.

Malale amemshukuru Waziri Biteko kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika hafla ya  uzinduzi wa Zahanati hiyo ambayo itapelekea kupunguza changamoto kwa wananchi wa kijiji hicho ambao hufuata huduma za afya umbali mrefu.

#women #WomenInMining #wanawakenamigodi 
#wanawakenamadini #malkiawamadini #tawoma 
#kaziinaendelea .

Our Blogs

Icon

MADINI YACHAGIZA MAENDELEO SEKTA YA AFYA

Read More
Icon

Women Contribution in the development in mining sector has to be recognized.

Read More
Icon

Lets partner to improve livehood of our artisanal women miners in Tanzania. 

Read More
Icon

What an honor and what a moment

Read More
Icon

Job Opportunity 

Read More
Icon

Job Opportunity

Read More
Icon

Unlocking possibilities :Empowering  women in mining and beyond.

Read More
Icon

SHINDANO LA MALKIA WA MADINI 2024

Read More
Icon

RECOGNITIONOFWOMEN CONTRIBUTIONINTHEMINERAL VALUE CHAININTANZANIA

Read More
Icon

UTAMBUZI WA MCHANGO WA MWANAMKE KATIKAMNYOROROWA THAMANI YAMADINIMIGODINI TANZANIA

Read More
Icon

Malkia wa Madini 2024

Read More
Icon

FINAL-ANNUAL REPORT 2023

Read More